Sad News: Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Abdalah Kigoda Afariki Dunia - LEKULE

Breaking

13 Oct 2015

Sad News: Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Abdalah Kigoda Afariki Dunia

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza na Mpekuzi siku chache zilizopita, alisema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi.


No comments: