14 Oct 2015

Burundi: zaidi ya watu saba wauawa Ngagara


Christophe Nkezabahizi mpiga picha wa runinga ya taifa ya RTNB tangu mwaka 1984, ameuawa na mke wake na watoto zake wawili (mmoja mwenye umri wa miaka16 na mwengine 14), Oktoba 13, 2015 Bujumbura.
Christophe Nkezabahizi mpiga picha wa runinga ya taifa ya RTNB tangu mwaka 1984, ameuawa na mke wake na watoto zake wawili (mmoja mwenye umri wa miaka16 na mwengine 14), Oktoba 13, 2015 Bujumbura.

Na RFI
Hali ya usalama inaendelea kudorora siku baada ya siku nchini Burundi, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Maeneo yanayoshambuliwa zaidi ni yale ambayo ni kitovu cha maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.
Jumanne Alaasiri, watu saba wameuawa wilayani Ngagara, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura, na wengine wengi wamejeruhiwa kwa risasi.
Kikosi cha ulinzi wa Rais kinanyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo. Mpiga picha wa runinga ya taifa ya RTNB Christophe Nkezabahizi, mkewe na watoto zake wawili ( mmoja mwenye umri wa miaka 16 na mwengine 14) ni miongini mwa watu waliouawa.
Wakati huo huo milio ya risasi imeendelea kusikika Jumanne jioni katika wilaya za Ngagara, Cibitoke, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura.
Polisi ilianza kuzingira maeneo hayo tangu saa 10:00 Alaasiri, na muda mchache baadaye milio ya risase ilianza kusikika.
Awali polisi ilikua ilikataa miili ya watu waliouawa wilayani Ngagara kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Christophe Nkezabahizi, ni mpiga picha kwenye runinga ya taifa ya RTNB tangu runinga hiyo ilipoanza kurusha matangazo yake hewani mwaka 1984.
Hata hivyo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katik mji wa Bujumbura, na miili ya watu wanaouawa inaendelea kuokotwa kila kukicha.

No comments:

Post a Comment