Christophe
Nkezabahizi mpiga picha wa runinga ya taifa ya RTNB tangu mwaka 1984,
ameuawa na mke wake na watoto zake wawili (mmoja mwenye umri wa miaka16
na mwengine 14), Oktoba 13, 2015 Bujumbura.
Na RFI
Hali ya
usalama inaendelea kudorora siku baada ya siku nchini Burundi, hasa
katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Maeneo yanayoshambuliwa zaidi
ni yale ambayo ni kitovu cha maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa
Rais Pierre Nkurunziza.
Jumanne
Alaasiri, watu saba wameuawa wilayani Ngagara, Kaskazini mwa jiji la
Bujumbura, na wengine wengi wamejeruhiwa kwa risasi.
Kikosi
cha ulinzi wa Rais kinanyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo. Mpiga
picha wa runinga ya taifa ya RTNB Christophe Nkezabahizi, mkewe na
watoto zake wawili ( mmoja mwenye umri wa miaka 16 na mwengine 14) ni
miongini mwa watu waliouawa.
Wakati
huo huo milio ya risasi imeendelea kusikika Jumanne jioni katika wilaya
za Ngagara, Cibitoke, Kaskazini mwa jiji la Bujumbura.
Polisi ilianza kuzingira maeneo hayo tangu saa 10:00 Alaasiri, na muda mchache baadaye milio ya risase ilianza kusikika.
Awali polisi ilikua ilikataa miili ya watu waliouawa wilayani Ngagara kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Christophe
Nkezabahizi, ni mpiga picha kwenye runinga ya taifa ya RTNB tangu
runinga hiyo ilipoanza kurusha matangazo yake hewani mwaka 1984.
Hata
hivyo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katik mji wa Bujumbura, na
miili ya watu wanaouawa inaendelea kuokotwa kila kukicha.
No comments:
Post a Comment