13 Oct 2015

AKINA MAMA WAJASIRIAMALI WAPAZA SAUTI ZAO

Akina mama wajasiriamali kutoka Wilayani Rorya ambapo kulia ni bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na bi.Magreth Steven. 

Akinamama wajasiriamali katika Kijiji cha Sota, Kata ya Tai iliyopo Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, wamewaomba wagombea watakaobahatika kuingia madarakani katika uongozi wa awamu ijayo, kuwakumbuka kwa kuwawezesha mitaji yenye riba na mashariti nafuu ili kuendeleza shughuli zao.
Walitoa ombi hilo wakati wakizungumza na Mtandao wa BMG (Binagi Media Group), uliowatembelea hivi karibuni ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na utunzaji wa mazingira zinazofanywa na wananchi katika ukanda wa Ziwa Victoria Wilayani humo.
“Sisi shughuli tunayoitegemea ni hii tu ya kuuza dagaa. Tunawafuata mwaloni (Mwalo wa Sota) na kuwaleta hapa (Mwamba dagaa) na kuwauza kwa watu wengine kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo nje ya Wilaya hii (Rorya) kwa ajili ya kwenda kutumia. Alisema bi.Winfrida Joseph ambae ni mmoja wa akina mama wajasiriamali zaidi ya 20 wanafanya shughuli zao za kuuza daa katika eneo la Mwamba daa na kuongeza;
“Kiukweli sisi hapa tuna changamoto ya ukosefu wa mitaji ya uhakika. Hivyo sisi ombi letu kwa hawa wagombea iwe diwani, mbunge au rais, yeyote yule atakaechaguliwa kuwa kiongozi, tunaomba atukumbuke. Atusaidie mitaji au kutuunganisha na taasisi zinazotoa mitaji yenye riba na masharti nafuu kwani masharti ya haya mabenki mengine yametushinda jamani”
Akinamama wengine akiwemo bi.Magreth Steven waliongeza kuwa wanaomba kuwepo kwa soko la dagaa la uhakika kama ilivyo kwa samaki katika mwalo huo wa Sota jambo litakalowasaidia kufanya biashara zao vizuri zaidi kwa kuwa hawana msaada mwingine zaidi ya kujishughulisha na biashara hiyo ambayo inawawezesha kupata mahitaji yao mhimu ikiwemo chakula pamoja na kuwasomesha watoto wao.
Wananchi wa Wilaya ya Rorya ambayo asilimia kubwa imetawaliwa na ukame kwa vipindi virefu vya mwaka, wanategemea zaidi shughuli za uvuvi ikilinganishwa na shughuli nyingine kama vile kilimo na uvuvi.

Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi


Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, Bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi.

No comments:

Post a Comment