MWENYEKITI
wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji (PICHANI) amenyakua
tuzo ya kielelezo cha viongozi wa biashara wa Afrika kwa mwaka 2015.
Manji
ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, aliwapiku
wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo bilionea namba moja Afrika,
Aliko Dangote.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi Quality Group, ilisema tuzo
hiyo ilimshtua 'bosi' wao kwani hakutarajia na kwamba itasaidia kuvutia
wawekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii
nchini. Tuzo hizo zilitolewa Septemba 16 mwaka huu.
Taarifa
hiyo iliongeza ya Manji ni chachu kwa vijana kufanya vizuri kwenye sekta
zao na itasaidia nchi kusonga mbele katika kujikwamua na umasikini.
Tanzania inaendelea kujukulikana kimataifa na itasawaidia watanzania kwa
ujumla kufanya kazi ama biashara katika nchi nyingine bila ya vikwazo
visivyo na msingi kupitia tuzo hiyo.
Baadhi ya
waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Emirates Group, Sheikh
Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege ya Emirates
inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na
nyingine kubwa.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Emmar Properties, Mohammed Alabbar pia bilionea kutoka
India, Ratan Tata anayemiliki kampuni kubwa yaEmeritus of Tata Sons Ltd.
Pia
bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri, Mukesh Ambani ambaye ni
mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni Yingluck Shinawatra,
Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
Pamoja na
ushindi huo wa kishindo wa Manji, pia kampuni yake ya Quality Group
imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa uhakika kwa bara la
Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”
No comments:
Post a Comment