20 Sept 2015

WASHINDI NDONDO CUP WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Kutoka kulia: Mke wa Dr. Mwaka (Mrs. Mwaka) na Shaffih Dauda (wapili kutoka kulia) wakimkabidhi katibu mkuu wa Faru Jeuri (kushoto) kiasi cha shilingi milioni tano wakiwa ndio mabingwa wa Ndondo Cup msimu huu
Kutoka kulia: Mke wa Dr. Mwaka (Mrs. Mwaka) na Shaffih Dauda (wapili kutoka kulia) wakimkabidhi katibu mkuu wa Faru Jeuri (kushoto) kiasi cha shilingi milioni tano wakiwa ndio mabingwa wa Ndondo Cup msimu huu
Waandaaji na wadhamini wa michuano ya Dr. Mwaka Sports Extra Nondo Cup iliyomalizika hivi karibuni, clinic ya Foreplan kwa kushirikiana na chini ya Dr. Mwaka na Sports Extra ya Clouds FM jana wamekabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyo pamoja na zawadi binafsi kwa washindi wa zawadi hizo.
Zawadi hizo zimekabidhiwa kwa washindi kwenye ofisi za Clouds Media Group majira ya saa tano asubuhi baada ya taratibu zote za utoaji zawadi hizo kukamilika kwa asilimia zote.
Ashindi wa michuano hiyo timu ya Faru Jeuri imejichukulia kitita cha shilingi milioni tano, washindi wa pili timu ya Kauzu FC wametwaa shilingi milioni tatu huku washindi wa tatu timu ya Makumba FC wao wakipata shilingi milioni mbili kwa kuibuka washindi wa tatu.

Zawadi nyingine zilitolewa kwa kikundi bora cha ushangiliaji ambayo imekwenda kwa kikundi cha Kauzu FC, mfungaji bora akiwa ni Idd Mbaga, mwamuzi bora na golikipa bora wote wakijinyakulia vitita vya shilingi laki tano (500,000) kila mmoja

No comments:

Post a Comment