20 Sept 2015

VIDEO: Chadema Yamvaa Bulembo Aliyesema CCM Haiko Tayari Kukabidhi IKULU Kwa Wapinzani


KAULI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kwamba “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani” imezua mjadala.

Bulembo alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni za urais wa mgombea wa chama chake Dk. John Magufuli Kigoma.

“Serikali imefanya makosa mengi na Chama Cha Mapinduzi kimefanya makosa mengi lakini hakitofanya kosa la kuruhusu chama pinzani kuingia Ikulu,” alisema Bulembo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ngome ya UKAWA, Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kukemea kauli hiyo.

Pamoja na hivyo Mbowe aliitaka CCM kufuta kauli kwa kuwa ni ya uchochezi ambayo inatoa tafisiri ya kutokuwepo umuhimu wa kufanya uchaguzi.

Mbowe alisema kuwa, tangu kutolewa kwa kauli hiyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na NEC wala kiongozi yoyote wa CCM aliyekemea au kuzungumzia na kuwa “inaonekana ni mipango ya chama hicho.”

Alisema kuwa, kauli hiyo ingetolewa na chama pinzani NEC isingevumilia na ingechukua hatua haraka.

Hata hivyo alisema CCM inalindwa na sheria mbovu na kandamizi na kuwa, zinahitajika kuondolewa.

Alifafanua kuwa, mfano wa sheria hiyo ni kutangazwa kwa matokeo ya urais ambapo kwa mujibu wa sheria hayapingwi mahakamani.

Msikilize  Mbowe  akiongea  hapo  chini




No comments:

Post a Comment