19 Sept 2015

TANZIA: MAREHEMU ESTHER GLORY MALONGO WA ATHENS, GREECE


Familia ya Marehemu George na Mama Rhoda Malongo wa Upanga, Dar es Salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa Esther Glory Malongo (pichani) kilichotokea ghafla tarehe 16/09/2015 kule Athens, Ugiriki. (1 Timothy 4: 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.)
Esther ataagwa na jamii ya Watanzania waishio Ugiriki siku ya Jumanne tarehe 22 September 2015. Halafu anategemewa kusafirishwa kutokea Ugiriki siku ya Alhamisi, tarehe 24 September 2015. Mazishi yanatarajiwa kuwa Jumamosi ya tarehe 26 September 2015 jijini Dar es Salaam Tanzania.
Mipango ya kuusafirisha mwili inaendelea kule Athens, Ugiriki. Msaada wa hali na mali unahitajika sana ili kuweza kufanikisha zoezi hili. Unaweza kutuma hela kupitia Western union, Athens, Greece kwa Ms Edna Neilly Malongo.
Kwa Mawasiliano zaidi:-
Edna Malongo +30 694 922 8337
au +255 784 600 577 (whatsApp only )
Tunatanguliza shukrani nyingi kwa upendo na ushirikiano wenu, Mungu na awabariki sana na akanyanyue watu wa kuwasaidia wakati mkihitaji msaada.

No comments:

Post a Comment