Kafando alizuiliwa wanajeshi walinzi wa rais walipovamia mkutano wa baraza la mawaziri
Rais wa
mpito wa Burkina Faso Michel Kafando aliyeondolewa mamlakani na kikosi
cha walinzi wa rais ameachiliwa huru na yuko buheri wa afya, viongozi wa
mapinduzi wamesema.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu Isaac Zida, aliyezuiliwa wakati mmoja na walinzi hao
walipovamia mkutano wa baraza la mawaziri, amewekwa kwenye kizuizi cha
nyumbani.
Viongozi
hao wa mapinduzi wamekubaliana kuhusu mambo muhimu ya kujadiliwa, huku
marais wawili wa mataifa ya Afrika Kusini wakiwasili nchini humo
kuongoza mashauriano.
Rais
Macky Sall wa Senegal na Thomas Boni Yayi wa Benin, walielekea Burkina
Faso kufanya mashauriano na viongozi waliopindua serikali.BBC
Sall alipakia mtandaoni picha iliyomuonyesha akiwa kwenye ndege safarini kuelekea Burkina Faso
Rafiki wa
karibu wa kiongozi wa zamani Blaise Compaore anayeishi uhamishoni Ivory
Coast, Jenerali Gilbert Diendere, alitangazwa kiongozi mpya na walinzi
hao Alhamisi.
Viongozi wa Amerika, Ufaransa na Muungano wa Afrika (AU) wameshutumu mapinduzi hayo.
Watu
watatu wanadaiwa kuuawa baada ya wanajeshi wa kikosi hicho cha walinzi
maalum wa rais (RSP) kuwakabili waandamanaji katika jiji kuu la
Ouagadougou.
Watu wamekuwa wakiandamana Ouagadougou kupinga mapinduzi hayo
Shirika la kijamii lenye ushawishi mkubwa la Balai Citoyen limesema waliouawa ni 10.
Idadi isiyojulikana ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo pia wamekamatwa na kuzuiliwa.
Viongozi hao wa mapinduzi wametangaza amri ya kutotoka nje usiku nchini humo na kufunga mipaka yote ya taifa hilo.
No comments:
Post a Comment