Mwakilishi
wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto)
akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta
mpakato zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya
ya Msingi ya Kakuni iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo
jijini Dar es salaam. Shule hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia wazo la
Wazo la Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya
kisasa katika kijiji hicho na inajengwa kupitia michango na misaada ya
wadau mbalimbali.
Mwakilishi
wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto)
akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa ‘Tablet’
100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya
Msingi ya Kakuni iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
Afisa
Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe.
Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya
michezi vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Mwenyekiti
na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG)
kilichopo mkoani Dodoma Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu
Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho kusaidia
wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha
Kibaoni mkoani Katavi .
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa
kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali
vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya
msingi Kakuni mkoani Katavi, ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30
vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi
Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.(Picha/ Aron
Msigwa-MAELEZO).
No comments:
Post a Comment