20 Sept 2015

Makamba: Watanzania Mchagueni Magufuli


KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amewaasa Watanzania kutofanya makosa kwa kumchagua Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa Rais wa Tanzania na badala yake wamchague Dk John Magufuli ambaye ni kiongozi makini anayejali shida za wananchi.

Akizindua kampeni za Jimbo la Mtera Kijiji cha Nagulo Kata ya Mpwayungu, Makamba alisema Dk Magufuli ni kiongozi anayekerwa na matatizo ya watu na kuyatatua.

Makamba alidai kuwa mgombea wa Chadema anadai kukerwa na matatizo ya watu, lakini wakati akiwa Waziri wa Ardhi alipora Ranchi ya Mzeli na kuifanya yake na familia yake.

Alisema hakuna zawadi nzuri, itakayoonyesha shukrani kwa Rais Jakaya Kikwete kwa mema aliyoyafanya katika uongozi wake, zaidi ya kuchagua viongozi wanaotokana na CCM kuanzia nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

“Livingstone Lusinde nimemlea mwenyewe, najua utendaji wake wa kazi na jimbo la Mtera limesikika na kupata umaarufu kwa sababu yake, hivyo ni vyema mkamchagua tena ili aendeleze na kumaliza yale aliyoyaanza,” alisema.


Kwa upande wake, Lusinde aliwataka viongozi wa dini waiombee nchi ili uchaguzi ufanyike kwa amani na kutoa mwito kwa viongozi wote dini nchini kuomba ili uchaguzi umalizike kwa amani na Rais bora apatikane.

No comments:

Post a Comment