18 Sept 2015

MAGUFULI AAHIDI KUDUMISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mjini Kibondo kwenye uwanja wa Taifa  katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo na kuhudhuriwa na Malefu ya wananchi mkoani Kigoma.
Dk. John Pombe Magufuli  akizungumza na wananchi wakati akiomba kura katika kijiji cha Mnanila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma Dk. Magufuli amesema serikali yake itaendeleza uhusiano wa Kidiplomasia na mataifa na nchi mbalimbali pamoja na  nchi majirani zinazoshirikiana na Tanzania katika nyanja za Uchumi, Utamaduni na Siasa.
Ameongeza kwamba ni muhimu kuendeleza ushirikiano  ambao umejengwa na marais wetu wastaafu waliopita na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi wetu katika nchi zetu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uchumi wa wananchi wa mataifa haya unakuwa kutokana na ushirikiano wa biashara na masuala mbalimbali ya kisiasa na kiutamaduni
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi katika kijiji cha Mnamila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
3
Umati wa Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Taifa mjini Kibondo jioni ya leo.
4
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akipanda jukwaani tayari kwa kuwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Taifa mjini Kibondo leo.

5
Kada wa CCM Bw. Jamal Abdallah Tamim akipigia debe Mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe Injinia Atashasta Nditiye katika mkutano huo.
6
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe Injinia Atashasta Nditiye.
79
Baadhi ya wananchi wakisubiri msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli upite huku mabasi pia yakiwa yameegeshwa kando ya barabara.
10
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Taifa mjini Kibondo tayari kwa kuwahutubia wananchi mjini Kibondo.
12
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagembea ubunge wa Kasulu Daniel Nsazugwako kulia na Agustino Zuma Ole katikati.
13
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli awahutubia wananchi wa Kasulu katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Umoja.
14
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
1516
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli ukisubiriwa kuwasili kwenye uwanja wa Umoja mjini Kasulu.
17
Kila mahali ni picha za Magufuli tu.
18
Akina mama wakifurahia hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli mjini Buhigwe.
19
Mama huyu akimfurahia Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwasalimia wananchi akiwa  njiani kuelekea mjini Kasulu huku akiwa amebeba mkungu wa ndizi.
20
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kijiji cha Mnamila wilayani Buhigwe.
21
Kikundi cha wanakwaya kikiwa tayari kwa kutumbuiza katika mkutano wa Dk John Pombe Magufuli katika kijiji cha Mnamila.
22
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akifurahia na mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe Mh Obama.
23
Ilikuwa ni furaha kwa watoto hawa kumuona Dk John Pombe Magufuli.
2425
Watu waliowengi walijipamba picha za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kila alipokuwa akipita na kuzungumza nao katika jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment