Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati) akishangiliwa na wananchi wenye ujumbe wa kumuunga mkono  huku akiwa na mfano wa msumeno wa kuwakatia wezi na mafisadi  akishinda urais wakati wa mkutano wa kampeni  mjini Igunga , Tabora jana. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Barafu mjini Igunga mkoani Tabora. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mtoto akiwa amebebwa na babake ili aweze kumuona Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM katika Kijiji cha eneo la Njia Panda Wilayani Maswa.
 Mama akishangilia kwa furaha huku akiwa amembeba mtoto wakati msafara wa Dk Magufuli ulipowasili eneo la Njia Panda wilayani Maswa jana.
 Mgombea ubunge Jimbo la Maswa kupitia CCM, Stanslaus Nyongo akijinadi kwa wananchi kwenye Uwanja wa Mpira mjini Maswa ambapo pia Dkt. Magufuli alifanya kampeni.
 Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa kampeni za CCM Mjini Maswa.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Maswa ili achaguliwe kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu
 Furaha ya mama huyu ilionekana dhahhiri baada ya kumuona Dk Magufuli katika Kijiji cha Malampaka wilayani Maswa, mkoa wa Simiyu jana.
 Dk Magufuli akizungumza na wananchi wakati akijinadi  mjini Malampaka, Maswa, ambapo alisema akishinda urais ataanzisha viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao nchini.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Suleiman Nchambi msafara wake ulipozuiwa na wananchi katika Mji wa Mwigumbi wilayani Kishapu Mwanza.
 Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwigumbi  Kishapu mkoani Shinyanga.
 Dk Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Maganzo mkoani Shinyanga, ambapo aliomba kumpigia kura ali ashinde awasaidie kuboresha sekta ya uchimbaji madini kwa serikali kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo  kwa kuwapatia mitaji  na vifaa.
 Mfanyabiashara akiwa amebandika mabango ya kampeni za Dk Magufuli na mgombea ubunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi
 Kikundi cha vichekesho cha Futuhi kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kishapu.
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi na kuelezea jinsi serikali ya CCM itakavyoboresha sekta mbalimbali nchini.
 Wasanii wakimsikiliza Dk Magufuli akijinadi mjini Kishapu.
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika  Kijiji cha Igurubi wilayani Magu.
 Sehemu ya umati wa wanaachi katika mkkutano wa kampeni za Dk Magufuli mjini Igunga.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdalah Bulembo akielezea wasifu mzuri wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli na kuwaomba wananchi kumpgia kura nyingi ili ashinde urais.
 Dk Magufuli akiwa na mfano wa msumeno aliopewa na wananchi ili utumike kuwakatakata mafisadi na wabadhilifu wa mali za umma.
Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM wilayani Igunga jana.