21 Sept 2015

Chama cha Syriza chashinda:Ugiriki



Alexis Tsipras akishangilia ushindi Ugiriki

Chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki cha Alexis Tsipras kimerejea tena madarakani nchini humo baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi.
Kwa kura nyingi zilizopigwa, hazikuweza kutoa viti vya kutosha bungeni kwa chama hicho kuunda Serikali huku Waziri mkuu Tsipras akiwa tayari amekubali kuungana na mrengo wa kulia kuunda serikali.
Tsipras amesema kuwa Ugiriki ilikuwa na kipindi kigumu lakini waliweza kupigana ndani ya Ugiriki na hadi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya na kwamba wataendelea na mapambano kuikwamua Ugiriki.
Kulikuwa na furaha miongoni mwa wafuasi wa chama hicho katika mji wa Athens.
Kiongozi wa chama cha New Conservative Vangelis Meimarakis amekubaliana na matokeo hayo,na kutoa tamko rasmi la kuunga mkono ushindi huo.
Akizungumza nje ya makao ya chama chake amesisitiza kuundwa serikali madhubuti.