18 Sept 2015

Burkina: upinzani na vyama vya kiraia vyajipanga baada ya mapinduzi


Mwana mitindo wa rap Martin Bambara, almaarufu Smockey, ni kiongozi wa shirika la kiraia la Balai citoyen, hapa ni kwenye eneo la Taifa katika mji wa Ouagadougou, Septemba 16, 2015.
Mwana mitindo wa rap Martin Bambara, almaarufu Smockey, ni kiongozi wa shirika la kiraia la Balai citoyen, hapa ni kwenye eneo la Taifa katika mji wa Ouagadougou, Septemba 16, 2015.

Na RFI
Jenerali Gilbert Diendéré, mkuu wa kikosi cha ulinzi wa (RSP), ameipindua serikali na kuchukua uongozi wa nchi ya Burkina Faso. Lakini mashirika ya kiraia na vyama vya siasa vimeapa kutokubali mapinduzi hayo ya kijeshi. Katika nchi nzima, mashirika ya kiraia na upinzani wamesimama, hasa katika vijana ili kutokubaliana na mapinduzi hayo ya kijeshi.
Chini ya mwaka mmoja baada ya maandamano yaliyomnga'tua madarakani Blaise Compaoré, na wakati ambapo demokrasia nchini Burkina Faso imekua ikionekana ikianza kujidhatiti, zikisalia siku chache kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge Oktoba 11, mapinduzi ya kijeshi yanauweka hatarini mchakato huo.
Tangu Jumatano usiku wiki hii, raia wa Burkina Faso waliingia mitaani ili kuonyesha ghadhabu zao dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP). Tangu mapinduzi ya kijeshi kutangazwa, mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na shirika la Balai Citoyen, yamekua yakitolea wito raia wa Burkina Faso na jeshi kutetea demokrasia yao. Katika mikoa, wito umeitikiwa, hasa kwa vijana wa Burkina Faso. Nchini kote, vijana ndiowameonekana mitaani Alhamisi wiki hii, wameandamana pamoja na mashirika ya haki za binadamu , na vyama vya mbalimbali vya wafanyakazi.
Katika mji wa Bobo Dioulasso, mji wa pili nchini humo, raia wameandamana bila hata hivyo kusubiri tangazo la mapinduzi ya serikali. IWaandamanaji hao wamekua wakisema: "mumuachiliye huru Zida" " mumuachiliye huru Kafando". Arsène Kamsie ni kiongozi wa harakati za vijana katika mji wa Bobo Dioulasso amesema: "tumeanza kujianda ili kupinga mapinduzi haya, kwa sababutunahisi kwamba wametusaliti. "
Nyumba ya Dienbéré yachomwa kwa moto
Hakuna maduka yaliofunguliwa vivyo hivyo katika mkoa wa Ouahigouya, Kaskazini-Magharibi na katika mkoa wa Tenkodogo, katikati mwa nchi. Kila mahali, shughuli mbalimbali zimekwama katika miji tofauti: kama katika mji wa Banfora, karibu na mpaka na Côte d'Ivoire: wakaazi wameweka vizuizi barabarani.
Katika mji wa Yako alikozaliwa jenerali Gilbert Diendéré, nyumba kadhaa zimechomwa, ikiwa ni pamoja na nyumba ya mkuu huyo wa kikosi cha ulinzi wa Rais aliyeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi.

No comments:

Post a Comment