20 Sept 2015

Burkina Faso: wasuluhishi wa Afrika waendelea na mashauriano


Michel Kafando (katikati) akizungukwa na Marais Boni Yayi na Macky Sall, Jumamosi Septemba 19, 2015.
Michel Kafando (katikati) akizungukwa na Marais Boni Yayi na Macky Sall, Jumamosi Septemba 19, 2015.
Na RFI
Baada ya kukutana na Rais Michel Kafando, akiambatana na Rais wa Benin Boni Yayi, Rais wa Senegal ametoa taarifa kuhusu hali inayoendelea nchini Burkina Faso, siku mbili baada ya mapinduzi ya jenerali Gilbert Diendéré. Kwa mujibu wa Macky Sall, njia kuondokana na mgogoro huo imeanzishwa na inaweza kutangazwa Jumamosi hii.
" Nimekuja na Rais Boni Yayi kumtembelea Rais Kafando. Kama mnavyonajua, tuliomba kuachiliwa kwake mara baada ya tukio la Jumatano 16. Jenerali Diendéré alituhakikishia kuwa ataterkeleza ombi letu. Kwa kweli tumekuja kumuona sisi wenyewe ili kuhakikisha ukweli huo. Tummezungumza kwa kina na Rais Michel Kafando kuhusu hali hii, vilevile kuhusu hatua za dharura zinasopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kurudi katika hali ya kawaida ", amesema Rais Macky Sall.
" Kwenda katika uchaguzi mapema iwezekanavyo "
Sasa hivi tutampokea jenerali Diendéré, na hapo itakuwa mwisho wa mazungumzo. Tangu Ijumaa wiki hii, mlifuatilia kama sisi, pande zote zilisikilizwa, tuna plani ambayo tumeanzisha, ni matumaini yetu kwamba ifikapo mwishoni mwa alasiri, tunaweza kuwa wazi zaidiikiwa ni pamoja na wananchi wa Burkina Faso, wanasiasa kutoka tabaka mbalimbali, vyama vua kiraia, Umoja wa Mataifa, ECOWAS na jumuiya ya kimataifa, tunaweza kusaidia hii kuondokana na hali hii ngumu, na kuendelea na mchakato wake wa mpito na kwenda kwenye uchaguzi mapema iwezekanavyo, "amesema Macky Sall katika mkutano na vyombo vya habari kuhusu hali inayoendelea nchini Burkina Faso.
Aidha, jeshi la kawaida la nchi hiyo limetoka katika ukimya wake. Mkuu wa majeshi ametoa tangazo Jumamosi lenye uangalifu, ambapo amesema jeshi la Burkina Faso haliungi mkono mapinduzi ya kijeshi na kuwa linajitenga na uamzi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP). Jenerali Pingrenoma Zagre amekumbusha kwamba jeshi linaungana na wananchi pamoja na maandili ya taifa. Pia amelaani vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya raia. Amehakikisha kuwa jeshi katika masaa ya kwanza ya mgogoro huo, lilijikubalisha pamoja na wadau wa kitaifa na kimataifa katika kutafuta ufumbuzi kwa ajili ya amani na usalama.
Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi ulikua mfupi, lakini "mazungumzo" hatua kwa hatua yameanzishwa Jumamosi asubuhi Septemba 19, amearifu mwandishi wetu ambaye yuko katika mji wa Ouagadougou, Guillaume Thibault, akiongeza kuwa shughuli za kidiplomasia zimeendelea kuongezeka katika chumba cha hoteli Laico Ouaga ambapo Macky Sall amefikia. Thomas Boni Yayi aliwasili katika hoteli hiyo wakati wa mchana Jumamosi mwishoni mwa huma hili. Akiwa ameghadhabishwa na hali inayoendelea nchini Burkina Faso, yayi Boni ameungana na mwenzake wa Senegal katika mashauriano hayo.
Viongozi hao wawili kisha walirejea katika hoteli hiyo kuendela na mazungumzo, ambapo walishiriki tangu saa 3:30 wanasiasa vigogo kutoka vyama mbalimbali, na hasa wa wapinzani wa Blaise Compaoré. Miongoni mwa waliokuwepo ni Ablassé Ouedraogo, Bénéwendé Sankara, Roch Marc Christian Kaboré, Saran Sérémé na Zéphirin Diabré. Wote walikuwa wagombea katika uchaguzi wa rais ulipangwa kufanyika mapema Oktoba, na wote walilaani jaribio la mapinduzi ya kijeshi, na wameendelea kulaani jaribio hilo mbele ya wapatanishi.
Wakati huo huo, maandamano yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Burkina Faso, ambapo watu 10 wanaarifiwa kuuawa na wengine 108 wamejeruhiwa.

No comments:

Post a Comment