24 Sept 2015

Breaking News: Waziri Celina Kombani afariki dunia



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India  alikokuwa akipatiwa matibabu

Taarifa tulizozipata usiku huu  zimesema  kuwa Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu

Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu.