22 Sept 2015

Bomu Lalipuka Ikulu Somalia, Lauwa 6

Wapiganaji wa IS Somalia
BOMU lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu. Takriban watu sita wamefariki, ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa.
Hata hivyo watu wengine 10 waliripotiwa kujeruhiwa. Mkutano kuhusu hali ya baadaye ya uchaguzi nchini humo umekuwa ukiendelea katika jumba hilo,lakini ulikuwa umeisha wakati wa mlipuko huo.

Wajumbe wengi waliripotiwa kuondoka katika eneo la jumba hilo. Hoteli moja karibu na jumba hilo iliharibiwa.