18 Sept 2015

Benki ya Posta Tanzania Yakabidhi Kituo cha Afya Pemba


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa PIli wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe: Hassan Khatib Hassan, mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ungi Mkusa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimia na viongozi mbali mbali wa Benk ya Posta Tanzania mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bwana Sabasaba Moshingi wakati alipowasili katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Mwanakijiji wa Ungi Msuka Mwadini Habibu akisoma risala ya wanakijiji hicho, kabla ya kuwekewa jiwe la msingi kituo cha Afya kilichopo kijijini kwao huko Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, Ismail Ali akitosa salamu za wanajumuiya wenzake wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya kijijini kwao huko Ungi Msuka.
Meneja wa Benki ya Post Tanzania tawi la Pemba, Issa Abdull akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungu Msuka Wilaya ya Micheweni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benk ya Posta Tanzania Bwana Sabasaba Moshingi, akisoma risala ya Benk hiyo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha Afya Ungu Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benk ya Posta Tanzania Profesa Lettice Rutashobya, azungumza na wanakijiji wa Ungi Msuka kabla ya kuwekwa kwa Jiwe la msingi Kituo cha afya kijijini hapo
Waziriwa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wapili kutoka kulia mwenye miwani akiangalia ratiba ya shuhuli ya uwekaji wa jiwe la Msingi kituo cha afya katika kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Watendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya znaizbar, wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment