Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa Lamaliza Mikutano yake kwa Kishindo. - LEKULE

Breaking

16 Sept 2015

Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa Lamaliza Mikutano yake kwa Kishindo.

Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa akigonga nyundo maalum kuashiria kukamilika kwa Mikutano ya Baraza hilo ambalo ameliongoza kwa mwaka  mzima. Kushoto kwake  ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa mwenye furaha wakati wa kuhitimishwa  Baraza la 69 ambapo alimpongeza Bw. Sam Kutesa kwa kuliongoza  Baraza kwa uhodari  uliopelekea kupitishwa kwa maazimio mbalimbali.

Na MwandishiMaaalum New York
Mkutano wa  69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  

uliokuwa chini  ya Urais wa  Waziri wa Mambo ya Nje wa 

Uganda Bw, Sam Kutesa umefikia ukingoni siku ya jumatatu 

kwa kupitisha maamuzi ya kihistoria ambayo pamoja na 

mambo mengine yanatoa mwelekeo wa majadiliano kuhusu 

marekebisho na mageuzi ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja 

wa Mataifa.

Maamuzi hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanaingizwa 

rasmi katika nyaraka muhimu za Baraza Kuu la Umoja wa 

Mataifa na yaliyopewa namba A/69/L.92 yalipitishwa kwa 

kauli moja na wajumbe kutoka nchi 193 wanaounda Baraza 

Kuu la Umoja wa Mataifa.

Maamuzi hayo ambayo baadhi ya wazungumzaji 

waliyapachika jina kama maamuzi ya Kutesa ikiwa ni ishara 

ya kutambua mchango wake katika kusimamia kidete 

majadiliano kuhusu mageuzi ya Baraza Kuu la Usalama la 

Umoja wa Mataifa yanatoa msingi  au maandishi ambayo 

yatawawezesha Nchi Wanachama kujadiliana kwa kupitia 

maamuzi hayo.

Ingawa maamuzi hayo yamepita bila  kupigiwa kura na 

kupongezwa kwa kufungua ukursa mpya katika kuendeleza 

mchakato wa majadiliano ya mageuzi na upanuzi wa Baraza 

Kuu la Usalama,  baadhi ya nchi zimeyaelezea maamuzi hayo 

kuwa ni ya kiufundi zaidi na hivyo yasikuchukuliwe kama 

maamuzi ya mwisho kwa madai kwamba, maandalizi na 

majadiliano ya maamuzi hiyo hayakuwajumuisha na hivyo 

hayawakilishi nina hisia za makundi yote.



Akiungana na wazungumzaji wengi waliounga mkono 

kupitishwa kwa maamuzi hayo Mwakilishi wa Kudumu wa 

Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi 







Akasema hapana shaka kwamba majadiliano   Zaidi 

yanapaswa kuendelea ili kujibu kiu ya kila upande na 

kwamba nchi wanachama wanapaswa kujivunia hatua 

hiyo muhimu hata kama ni hatua ndogo.
Akatumia fursa hiyo kuwapongeza Bw.Sam Kutesa na 

Mwakilishi wa kudumu wa Jamaica Balozi Rattray kwa kazi 

nzuri , kubwa na iliyokuwa na changamoto nyingi lakini 

iliyofanikisha kupatika kwa maamuzi hiyo.

Majadiliano kuhusu namna ya kuboresha na kupanua 

wigo wa wajumbe wa Baraza Kuu la  Usalama la Umoja 

wa Mataifa, ni majadiliano yaliyoaza mwaka 2008 lakini 

ni katika Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa 

Mataifa ambapo matokeo ya majadiliano miongoni mwa 

wanachama yameweza kupitishwa rasmi katika Baraza 

Kuu la  Umoja wa Mataifa.

Muundo wa sasa wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja 

wa Mataifa ambalo lina wajumbe wakudumu na wenye 

kura ya turufu watanona wajumbe  10 wanaoingia kwa 

mzunguko wa uwakilishi wakiandaa haujaitendea haki 

Afrika  bara ambalo lilokumbwa kwa asilimia kubwa ya 

maamuzi yanayofanywa na Baraza Kuu la  Usalama 

yanaihusu Afrika lakini Afrika si mwanachama wa 

kudumu na hiyvo imekuwa ikipigania kupata nafasi ya 

uwakilishi wa kudumu pamoja na kura ya turufu.

Kumalizika kwa Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la  

Umoja wa Mataifa,  kunafungua kuanza kwa Mkutano 

wa Baraza Kuu la 70 ambalo kwa mwaka mzima 


litakuwa chini ya Urais wa Bw.Monges Lykketoft.

No comments: