Wema Isaac Sepetu.
HALI si
shwari kwenye familia ya Kampuni ya Endless Fame Productions kufuatia
madai mazito yanayomgusa mkurugenzi wake, Wema Isaac Sepetu akihusishwa
na kuvunjika kwa ndoa ya mdogo wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz aliyeolewa na
Hamad Manungwa ‘Petit Man’.
Mdogo wa mkali wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ almaarufu kwa jina la Esma Platnumz
akiwa na mume wake Hamad Manungwa ‘Petit Man’ siku walipofunga ndoa.
MAI NDANI
Katika sakata hilo, mtangazaji maarufu
Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’, Esma na Mtangazaji Nasra Rajesh ‘Lady Naa’
wanadaiwa kuunda kundi lenye lengo la kuwasuta wezi wa waume za watu
(Wema aliwekwa kwenye tageti) lililopewa jina la Al-Shabaab.
Esma Platnumz akiwa na mume wake Hamad Manungwa ‘Petit Man’.
Wakati mpango huo ukiendelea, Mai
anadaiwa alielezea mkasa wa kuvunjika kwa ndoa ya Esma na Petit Man
kwenye Instagram huku akimtaja Wema kuhusika kwa mafumbo, jambo
lililomfanya staa huyo wa filamu (Wema) aogelee matusi ya kutosha.
MADAI YA WEMA KUHUSIKA
Madai kamili yanamhusisha Wema na
uvunjifu wa ndoa hiyo akituhumiwa ‘kuchepuka’ na Petit Man kwa muda
mrefu sasa huku mwenyewe akikanusha vikali.
USHAHIDI WA MESEJI
Madai yalizidi kushushwa kwamba, sakata
hilo lina ushahidi ikiwa ni pamoja na Esma kubamba meseji zisizo na
dalili njema kutoka kwa Wema zikiwa kwenye simu ya Petit Man.
“Ukibahatika kukutana na Esma halafu
umkute kwenye ‘mood’ ya kuongea, atakueleza jinsi mume wake alivyokuwa
na ukaribu wa kupitiliza kwa Wema. Yawezekana hawakuwahi kuchepuka
lakini ukaribu wao ulikuwa wa kupitiliza kiasi cha kuibomoa ndoa hiyo.
SIMU ZA WEMA HADI USIKU WA MANANE
“Esma anadai kuwa kuachana kwake na
Petit Man hakuhusiani sana na meseji za Diva (Mtangazaji wa Clouds FM,
Loveness Malinzi) kwani hizo zilisherehesha ugomvi wao tu, ila
kilichomfanya hadi akaamua kubwaga manyanga ni utitiri wa meseji za
wanawake na simu kibao za Wema kumhitaji Petit Man hadi usiku wa manane
wakati ni mume wa mtu,” kilidai chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Kufuatia madai hayo, Ijumaa
lilimtafuta Wema alipopatikana alisema: “Mimi nimekuwa nikimsapoti
Petit kwenye mambo yake na Esma, sasa kama kuna watu wanasema maneno ya
kunifanya nionekane mbaya, hao ni watu wasio na nia njema na mimi.
“Nakaa na Petit kama mwanangu lakini pia
ni mfanyakazi wa Endless Fame na Esma sina tatizo naye, zaidi watu
wanaibua tu mambo yao. Sipendi kabisa…”
ESMA KIMYA
Esma alipotakiwa kufunguka juu ya madai
ya Wema kuhusika kwenye kuvunjika kwa ndoa yake alisema kwa kifupi:
“Hilo suala liko kwenye ngazi ya kifamilia, siwezi kuliongelea kwa
sasa.”
WEMA AKEREKA
Kufuatia maneno ya kuuma kwenye mtandao
aliyokuwa akiendelea kuandika Mai, Agosti 18, Wema alishindwa kuvumilia
hivyo kwenda kumripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama.
Paparazi wetu aliponyetishiwa ‘ubuyu’
huo wa Wema kulifikisha ‘soo’ hilo polisi, alinyanyua mguu hadi kituoni
hapo ambapo alikutana na askari wakiongozana na Wema hadi Mitaa ya
Sofani, Kijitonyama ambako kuna duka la Mai lakini hawakumkuta hadi
kesho yake (Jumatano asubuni) alipotiwa mbaroni.
MSIKIE MAI
Baada ya Mai kufikishwa kituoni hapo
alishikiliwa kwa saa kadhaa akihojiwa na alipotoka na kutakiwa kusema
chochote kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Huu ni mziki mnene, Wema amechokoza moto.”
PETIT MAN NA ESMA
Katika ndoa yao, Petit Man ambaye ni
mmoja wa wafanyakazi wa Endless na Esma wamedumu kwa takriban miaka
miwili na kujaliwa mtoto mmoja kabla ya mambo kwenda mrama hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment