Waziri
wa Nishati na Madini. George Simbachawene, akisisitiza jambo kwa
wanafunzi kabla ya kuwakabidhi Nyaraka za Ufadhili kwa ajili ya masomo
yao nchini China.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya Watumishi wa Wizara na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo katika ngazi za Shahada za Uzamivu (Phd) na Uzamili (Masters), katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.
Baadhi
ya wanafunzi 22 waliopata nafasi za masomo ya shahada za Uzamili na
Shahada ya Uzamivu wakimsikiliza kwa kwa makini Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene.
Waziri
akiwakabidhi nyaraka za kusafiria na zenye maelezo baadhi ya wanafunzi
waliopata ufadhili wa masoma katika masuala ya mafuta na gesi nchini
China.Katikakati ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli,
James Andilile.
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akiwakabidhi wanafunzi 22 wa Kitanzania Nyaraka za Ufadhili wa kusoma masuala ya mafuta na gesi nchini China.
Waziri
wa Nishati na Madini George Simbachawene, amewakabidhi Nyaraka
za Ufadhili na kuwaaga wanafunzi 22 wa Kitanzania wanaokwenda masomoni
nchini China, kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada
za Uzamivu (Phd) na Uzamili (Masters).
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi Nyaraka hizo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini
Dar es Salaam, leo, Simbachawene amewataka wanafunzi hao kutumia fursa
hiyo kusoma kwa bidii ili hatimaye waweze kusaidia Taifa katika
kuendeleza sekta ndogo ya gesi ikiwemo kuanzisha vyanzo mbadala vya
nishati ya umeme , kuongeza usimamizi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa
sekta hiyo, na kusaidia katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta
hiyo.
“Kama
mnavyoelewa Wizara yetu ni miongoni mwa Wizara zilizo katika Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika sekta ya Nishati. Mpango
huu unategemea kutoa matokeo makubwa ya haraka, na hili kutekeleza
ipasavyo tunahitaji wataalamu wazalendo waliobobea katika fani za
,mafuta na gesi asilia” alisema Simbachawene.
“Ni
matumaini yangu kuwa mtatumia vizuri fursa mliyopata, mtajifunza kwa
bidii na kuiwakilisha nchi yetu vizuri
na kuleta teknolojia zitakazosaidia kupata ufumbuzi au
mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta
hii”alieleza Simbachawene.
Aidha,
Waziri alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Jamuhuri ya
Watu wa China kwa kuwawezesha Watanzania kusoma masuala ya mafuta na
gesi tangu mwaka 2013 na kuongeza kuwa , serikali hiyo imeahidi
kuendelea kutoa ufadhili kwa watanzania katika ngazi za Shahada ya
Uzamivu na Uzamili hadi ifikapo mwaka 2019.
Aidha,
Simbachawene ameeleza kuwa, Wizara ilipokea jumla ya maombi 187 na kati
yao, waombaji 33 waliokidhi vigezo walichunjwa na Serikali ya Watu wa
China na kupatikana washindi 22.
Clinton Ndyetabula ni Mwanafunzi ambaye yuko katika Mafunzo ya Vitendo, Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment