Msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajenti’.
LICHA ya kukana mara kwa mara
kuhusu kuwa na ujauzito, kuna madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Husna
Idd ‘Sajenti’ amejifungua mtoto wa kike.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili
kwamba mwanamama huyo alijifungua hivi karibuni katika Hospitali ya
Kinondoni, maarufu kama Kwa Dokta Mvungi na kwamba jambo hilo analifanya
siri kwani hataki watu wajue kama amepata mtoto huyo wa pili.
Gazeti hili lilipomtafuta na kumuuliza
kuhusu madai hayo, alikataa katakata kuwa na mtoto, habari ambazo
zimewashangaza watu wake wa karibu, waliosisitiza kuwa habari hizo ni za
kweli na kwamba kwa sasa anaishi na mwanaye huyo kwa dada yake maeneo
ya Sinza, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment