Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada jana
jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria
mkutanoni.
Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu
mchakato mzima wa uchaguzi na hatua zilizofikiwa hadi sasa jana jijini
Dar es salaam wakati wa mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini.
Baadhi
ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC jana
jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.
Wanasekretarieti
ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali na baadhi ya
waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini
kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akiteta jambo na
mmoja wa makamishna wa Tume hiyo Prof Amon Chaligha jana jijini Dar es
salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau mbalimbali.
Tume
ya Taifa ya uchaguzi NEC imewaomba viongozi wa dini zote kutumia
majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea
upande wowote wa mgombea ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa
uchaguzi Mkuuu ujao.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye
Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao
wa uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika
kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema
kuwa taasisi za kidini zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika
kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa
watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na kuwaacha watanzania
wakiwa na umoja na mshikamano licha ya tofauti za kiimani zilizopo
miongoni mwao.
“Tume
inawataka, nyinyi viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi
kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama
chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema
chama au mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la
EAGT-Mikocheni -A ameiasa Tume hiyo kusimama katika haki, uhuru na
kuhakikisha wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo ili kuivusha
nchi ikiwa salama.
Mshiriki
mwingine kutoka Kanisa la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa
amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati huu wa
uchaguzi maana amani inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini
wao hivyo wao kama taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu
kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na viongozi hao na wadau wengine
ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa
ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao..
No comments:
Post a Comment