Untitled
Matumizi ya simu za kisasa (smartphones) yameonyesha kuongezeka kwa kasi ambapo zaidi ya Terabyte 76,000 hutumika kwa mwezi mmoja, hii imekuwa ni mara mbili ya takwimu zilizofanyika mwaka 2013 ambapo kulikuwa na matumizi ya TB 37,500 kwa mwezi mmoja katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara. (Ripoti ya Subsaharan Africa Ericsson Mobility, 2014).

Kwa upande mwingine , soko la simu za kisasa pia linakua kwa kasi, ambapo inaonyesha kuwa kutakuwa na ongezeko la mara mbili ya manunuzi ya simu za kisasa (smartphones) katika miaka miwili ijayo, ambapo Nokia, Samsung na Iphone ndizo zinanunuliwa kwa kasi katika miaka ya 2014/2015. CNN

Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania anafafanua kwamba, “Ongezeko la matumizi ya smartphones hapa Tanzania linauwezo mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi hasa kupitia biashara za mitandaoni,  kutokana na  muda mwingi wa watu wanautumia katika kuperuzi kwenye simu zao”.
Guzzoni alifafanua kuwa, “kwa kadri miaka inavyozidi kuendelea, hakuna mtu atakaye tafuta bidhaa au huduma yeyote bila ya kuanzia kwenye mtandao. Hii ni kutokana na sababu za kuokoa muda na kukua kwa ulimwengu wa kidigitali na utandawazi”.
“Faida au hasara za simu za kisasa inatokana na matumizi yake, watu wengi wameelimika na wengine hujipatia huduma bora kupitia mitandao, hivyo kuongezeka kwa matumizi ya smartphones isiwe kwa ajili ya kuporomosha uchumi au maadili, bali iwe ni changamoto katika kukuza uchumi wa nchi, mfano mzuri ni Nigeria ambao wako mbele katika matumizi ya smartphones lakini sana wamekuza sekta ya utalii, kupitia Jovago.com. Lilian Kisasa, Meneja Mawasiliano wa JovagoTanzania.
“Iwapo watumiaji wa simu za kisasa wanaendelea kuongezeka, hivyo hata wamiliki wa biashara mbali mbali wanahitaji kubadili muelekeo wa biashara au huduma zao; “Japan wanaendelea kukuza uchumi wao kwa kuuza zaidi ya 80% ya bidhaa zao kupitia mitandaoni, hivyo hivyo na nchi zinazoendelea katika maendeleo ya kukuza uchumi inabidi tukubaliane na hali halisi ya utandawazi kuwa masoko yanaingiliana na wasitegemee aina moja ya kutoa huduma” alifafanua”.
Kwa Mwaka 2014, Tanzania imeshika nafasi ya 9 kwa nchi za kusini mwa bara la Africa, na nafasi ya 2 kati ya nchi za Africa ya Mashariki kwa matumizi ya simu za mkononi, lakini pia inakadiliwa zaidi ya 25% ya watu wanaotumia smartphones wanapata huduma zao za malazi, chakula, elimu, na habari kupitia mitandaoni.