Albino 5 raia wa Tanzania waliokatwa viungo wamerejeshewa viungo bandia Marekani
Watoto
watano wa Tanzania wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya
miili yao wamewekewa mikono na miguu ya bandia katika hospitali iliyopo
nchini Marekani.
Watoto
hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini humo
ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa
shughuli za kishirikina
Watoto
hao, mmoja wa kike na wanne wa kiume kutoka mikoa ya Kaskazini Magharibi
na Kusini Magharibi mwa Tanzania, wamekuwa wakipokea matibabu hayo
katika hospitali ya watoto Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini
New York.
Wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Wakiwa na
umri kati ya miaka 6 hadi 18, wanne wa watoto hawa walipatwa na
majeraha makubwa ya kukatwa mikono na miguu yao, huku mmoja wao akiwa
amekatwa taya na meno.
Tayari
watoto wanne wamekwisha wekewa mikono na miguu ya bandia, wakati yule
aliyekatwa taya akitarajiwa matibabu yake kuchukua muda mrefu zaidi
Shirika la msaada la Kimarekani Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya watoto hawa.
Ofisa kutoka shirika la Under the Same Sun Martin Haule anasema watoto wanaendelea vizuri na kwamba ni wenye furaha
Shirika la Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya watoto hawa.
Ameiambia BBC kwamba wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulemavu wa ngozi unaathiri takribani mtu mmoja katika kila watu 15,000 nchini Tanzania.
Watu hawa wanawindwa kwa ajili ya viungo vyao, ambavyo vinatakiwa katika biashara haramu kwa matumizi ya shughuri za kishirikina
No comments:
Post a Comment