Serikali ya Nigeria na nchi nyengine
nne majirani zimekubaliana kuunda vikosi vya jeshi la pamoja ili
kupambana na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram.
Baada ya mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, katibu mkuu wa wizara ya ulinzi ya Nigeria, Aliyu Ismail, amesema kikosi hicho kitakuwa tayari kuanza kazi ifikapo mwezi July mwaka huu:"viongozi wa nchi na serikali za nchi za ukanda wa ziwa Chad na Benin zimechukua uamuzi ufuatao.
kupitisha dhana ya ufanyaji kazi, mikakati ya ufanyaji kazi na nyaraka zinazohusiana na kuundwa kwa vikosi vya pamoja katika kupambana na kundi la kigaidi la wapiganaji wa Boko Haram, kupitisha kupelekwa kwa vikosi hivyo katika makao makuu ya Ndjamena, Chad, kwa utekelezaji wa rasilimali watu na mahitaji ya kifedha.
No comments:
Post a Comment