Bunge laahirisha shughuli zake leo.
Bunge leo limeahirisha shughuli zake, baada ya kupokea taarifa za kifo cha mbunge wa Ukonga Bibi. Eugine Mwaiposa, aliyefariki dunia usingizini nyumbani kwake mjini Dodoma.
Akitangaza kifo hicho mbele ya wabunge wote wakati kikao cha bunge kikiendelea, Naibu Spika wa Bunge Bw. Job Ndugai alisema:
Kufuatia kutoka kwa kifo hicho ambapo mwili wa marehemu Mwaiposa utaagwa kesho siku ya jumatano, naibu spika ikambidi kuahirisha shuguli za bunge kama kanuni zinavyoongoza.
Mapema wakichangia hoja bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii, Msemaji wa kambi ya upinzani Dk. Anthony Mbassa ameitaka serikali kuzingatia ushauri inaopewa juu ya tatizo la mara kwa mara la uhaba wa dawa na vifaa tiba nchini.
Mapema akiwasilisha makadirio ya bajeti ya shilingi bilioni 813.9 kwa mwaka 2015/2016, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Selamani Rashid, amesema serikali itaendelea kuunganisha hosipitali mbalimbali nchini na mfumo wa tiba mtandao, kwa kuwa umeonyesha manufaa makubwa katika utoaji huduma.
No comments:
Post a Comment