Bondia wa Tanzania Fransic Cheka
anatarajia kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela mei
30.ambapo atacheza na bondia Kiatchai Singwancha kutoka Thailand
,pambano hili litakua la raundi kumi litakalofanyika katika ukumbi wa
P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam.
Akizungumzia maandalizi ya
pambano hilo Kaike Siraju ambaye ndiye mwaandaaji wa pambano amesema
kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa sasa ambapo
mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusaini mikataba wiki hili.Pambano hilo litasimamiwa na chama cha ngumi za kulipipwa Tanzania P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwa bondia Kiatchai atawasili nchini siku tatu kabla ya mpambano huo .
No comments:
Post a Comment