Ray C: Nimenenepa lakini kiuno bila mfupa kiko pale pale! - LEKULE

Breaking

26 Apr 2015

Ray C: Nimenenepa lakini kiuno bila mfupa kiko pale pale!


Rehema Chalamila aka Ray C amewatoa hofu mashabiki wa muziki wake, kuwa unene wake haujakiathiri kiuno chake bila mfupa bali kimemwongezea uwezo wa kukatika kuliko zamani!

Ray C ambaye alitamba na nyimbo kama ‘Sikuhitaji’ na ‘Umeniacha’, ameiambia Global TV kuwa anahisi uwezo wake wa kukatika umeongezeka zadii kutokana na unene.

“Sina tofauti na Ray C wa zamani,” alisema. Ray C ni yule yule, kiuno cha zamani ni kile kile. Sema sasa hivi kina nyama kidogo kwahiyo sasa hivi nikifanya kidogo tu yaani ni rahisi zaidi kwangu.”

No comments: