Oya masela inakuwaje hapo kwa kitaa yako. Kwani kuna mizinguo? Ama nini? Kama barida basi freshi chaliiangu.
Dah! Makachaa prezidaa wetu Jei Kei alikuwa na mzinguo f’lani wa kiafya bati wana wa Obamalendi wakafanya manuva akakaa mahali yake na wote tuseme dhenki yuu Godi kwa kumfanya awe fiti. Tumpe pole mzazi jembe arejee kwa fasi ya homu dheni tuendelee kulisongesha! Ama nini? Jiti!
Wanangu kitu cha mwaka ndo kama hivyo kinadisapia kwa spidi ya ajabu arifu. Unaambiwa pipo wapo kwenye mbishe za kupiga bingo ili wakafunge mahesabu kileji. Si unajua zile za kwenda kuhesabiwa? Aisee masti na mimi niruke kwa kileji nikakumbushie zile za kitambo.
Ebana tudei nina bonge la stori moo kutoka kwa sistaduu mmoko. Naomba nimtaje kwa hefufi Y kozi ameomba hifadhi ya neimu lake. Unajua kwa mastresi aliyonayo dheni ukimwongezea mengine ya kumtaja inamfanya akutane na msala mwingine kwenye sosayati.
Mara kibwena unakuta maduu, wasichana, mabinti na wachuchu wanasafa sana kwenye suala la malavu hasa pale makachaa wao wanapofeli kutimiza promisi walizowawekea.
Ebana kuna mameni wanajua kuimbisha aibu. Mara nitakujengea ghorofa, nitakununulia BMW kama la Wema…oooh…nitakununulia kisiwa na praiveti jeti…na mengine ya sampo hiyo ilimradi tu amnase.
Eti mwanangu Masta T eti hana hata jiti wala mishe za kumwingizia mawe dheni anamchiti shori atafunga naye mereji kwenye Visiwa vya Barbados kwa akina Rihanna! Si muujiza huo jamani wanangu?
Achana na promisi fekelo ambazo unajua kabisa hakuna ishu ka hiyo bati unamwona mwana anasukuma ndinga la gavamenti au praiveti kampani dheni shori anaamini ni la mwana! Huo si umbulula sasa!
Hicho ndo kilimkuta mtoto mkare pale kati. Mtoto Y amegroo kwenye laifu tafu kinoma hapo kitaa cha Singida. Alichofanikiwa kuwini ni kulinda usichana wake hadi akatimba tauni Bongo tambarare. Kwa wanyama wenyewe!
Mtoto akawa anapiga mbishe za kusaka bingo kwa kutoa sevisi kwa Mama Ntilie hapo kitaa cha Karume kwa fasi ya Dar baada ya kuhaso vya kutosha kupata sehemu ya kuchili na kumbonji.
Huku na huku anaibuka mwana anajifanya amemsoma na anataka kumpa laifu. Mwanzoni shori anaweka ngumu kinoma.
Kuna msemo wa wana kitaa kuwa hata simba ni mkali bati anazaa so hakuna shori anayeweza kupindua kwa msela anayejua kumingo. Unabisha? Waachie masela kifaa chako dheni utaambulia manyoya daadeki! Oya abiria chunga mzigo wako!
Unaambiwa kitendo cha yule shori kumkubalia selaa, fasta akajikuta akilosti respekti ambayo ni usichana wake! Chezea heshima ya kuweza kutunza kitumbua chako kisiingie mchanga? Kaa humu wewe upate mambo!
Dah! Wiki bee tu tayari mtoto mkare akawa pregi na katika kumseti selaa si ndo akaingia mitini? Sasa shori kajifungua! Dingi wa mkidi wake haonekani! Hana daireksheni, anaishi kwa kuungaunga. Ona sasa bata la siku moko tu limemkosti laifu lake!Mtoto Y ni sampo tu kozi nina kesi kibwena za mashori wanakrai deile kutokana na wana kuwazingua ilihali wao wanajitoa asilimia jiti.
Wanapozinguliwa wanapata mastresi kinoma. Mbaya zaidi akikumbuka zile promisi za kuolewa, kujengewa hausi, kupigwa skonga na nyingine kibwena na kujikuta wakilosti mahopu ya kuishi.
Bati haya yote husababishwa na mashori wenyewe kwani huwa hawajui wanachitiwa? Je, huwa hawajiulizi watachitiwa hadi lini? Eti wakishakutana na situwesheni kama hiyo akitokewa na meni utasikia wanaume ticha wenu ni mmoko.
Mashori acheni kulialia kwa kushindwa kujipanga. Shori tabasamu ndo mpango mzima. Ishu za kulialia iachie kengele! Kwa upande wa makachaa na ninyi acheni kucheza na mioyo ya watoto wa kike. Hivi mnanyaka huwa wanavyolia ni laana kwenu wanangu? Acheni hizo!
Mmenisoma? Kaa humu wewe! Kama vipi sii yuu neksti wiki!
No comments:
Post a Comment