Chelsea waongoza kwa utovu wa nidhamu England - LEKULE

Breaking

18 Apr 2015

Chelsea waongoza kwa utovu wa nidhamu England


Takwimu zilizotolewa na maafisa wa mchezo wa kiungwana wa FA zinaeleza kuwa Chelsea ni timu inayoongoza kutoheshimu maamuzi ya waamuzi katika ligi kuu England, huku makocha wa timu hiyo wakishika nafasi ya pili kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi.

Liverpool imetajwa kuwa klabu yenye heshimu kubwa kwa waamuzi katika kipengele hicho kilichobeba alama saba ikifuatiwa na Burnley na West Brom.

Klabu za Arsenal na Stoke City zipo katikati katika orodha hiyo ambapo kanuni zinaeleza kuwa kitendo cha kuheshimu maamuzi yenye utata bila kugoma au kumzonga muamuzi kinaipa timu alama saba wakati tabia ya kukubali maamuzi halafu kuonesha ishara za kutoheshimu zinatolewa alama sita.(P.T)

FA wanatoa alama kwa kuangalia maeneo sita ambayo ni kadi nyekundu na njano, mchezo mzuri, heshima kwa wapinzani, heshima kwa waamuzi, tabia ya maafisa wa timu na mashabiki.

Alama kumi zinatolewa kwa kadi nyekundu ambapo timu inapunguziwa alama moja kwa kadi ya njano na alama tatu kwa kadi nyekundu.

Mchezo mzuri una alama kumi zinazotolewa kwa kucheza soka la kuvutia, kushambulia sana na kushinda, lakini timu ikitumia mbinu za kujilinda na udanganyifu alama zinapunguzwa.

Alama saba zinatolewa katika kipengele cha heshima kwa wapinzani kinachohusisha kuwaheshimu wachezaji pinzani na kuonesha mchezo wa kiungwana, wakati alama saba pia zinatolewa kwa kuheshimu waamuzi na maafisa wa mechi.

Alama sita zinatolewa kwa maafisa wa timu wakiwemo makocha dhidi ya waamuzi, wakati alama kumi zinatolewa kwa tabia ya mashabiki ambapo alama zote zinatolewa kwa mashabiki wanaokubali matokeo, wakati wakitumia lugha ya matusi kwa wachezaji, waamuzi na kuwatishia mashabiki pinzani alama zinapounguzwa.

No comments: