Kikosi kazi,maalumu kilichoundwa na serikali, kufuatilia mwenendo wa mtandao wa ujangili nchini kimefanikiwa kuwakamata watuhumumiwa muhimu zaidi ya 40 na kuwaweka wengine chini ya uangalizi maalum, baada ya kuanza kwa operesheni hiyo mwaka 2013
Mratibu wa kikosi hicho katika eneo la ikolojia ya Serengeti,ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha kupambana na ujangili wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro (NCAA)Bw.Robert Mande amewaambia waandishi wa chama cha wanahabari za maliasili na utalii(TJT) kuwa hayo ni matokeo ya ushirikiano wa vikosi vya kuzuia ujangili,katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hifadhi ya Serengeti,Manyara na Tarangire.
Bw.Mande amesema tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na kazi ya kufatilia mtandao huo inaendelea licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na ukubwa na uzito walinao watuhumiwa wa mtandao huo.
Uchunguzi ulioshirikisha makundi mbalimbali wakiwemo wananchi wanaoishi jirani umeonyesha kuwa mtandao huo unajumuisha watu wa ngazi mbali mbali wakiwemo wataalam kuua tembo na kutoa meno kwa mudamfupi,madalali,na wamekuwa wakipewa mikopo yamagari, silaha na mahitaji mengine ya kufanya ujangili ili kufanikisha kazi hizo na kutoa rushwa kwa baadhi ya watendaji wanaojaribu kukwamisha kazi yao.
Kaimu meneja wa idara ya utalii wa mamlaka ya Ngorongoro Bw.Asanaeli Merita, amesema changamoto ya ujangili uliokuwa umeshika kasi hivi karibuni kwa upande mwingine imeongeza chachu ya udhibiti na umakini kwa kila idara na baadhi ya matokeo yameonekana yakiwemo kuongezeka kwa mapato.
Kati ya mwaka 2013 na 2014 Tanzania ilikumbwa na wimbi kubwa la ujangili hasa wa meno ya tembo ambao licha ya kwamba kwa sasa umedhibitiwa ulitishia uwepo wa wanyama hao na pia uchumi wa tanzania ambao kwa kiasi kikubwa unategemea sekta ya utaliii.
No comments:
Post a Comment