Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutolewa hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa baada ya kupoteza fahamu na kisha kupelekwa kituo cha Polisi oysterbay kwa ajili ya mahojiano.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi na kupewa dhamana, Gwajima amesema hawezi kutishika na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea wakristo nchini .
“Nimetoka kwa amani, nashukuru sana Mungu ameniponya,ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao wanakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
Askofu Gwajima amewataka viongozi wenzake kuheshimu tamko lililotolewa na Jukwaa la Kikristo Tanzania.
“Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu Tamko hili la kikristo na endapo tutakuwa tofauti basi tutakuwa tunapingana na msimamo wetu na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho” ameongeza Gwajima.
Alipoulizwa na waandishi wa Habari kuhusu Afya yake Gwajima amesema hawezi kuzungumzia Afya yake kwa sasa.
Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.

No comments:
Post a Comment