BREAKING NEWS:Wanajeshi 180 wa Kenya waliuawa na al-Shabab - LEKULE

Breaking

25 Feb 2016

BREAKING NEWS:Wanajeshi 180 wa Kenya waliuawa na al-Shabab


Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ametoa maelezo kuhusu idadi ya wanajeshi wa Kenya waliofariki kufuatia shambulio la al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde mwezi uliopita.
Rais huyo ametoa idadi hiyo kuwa kati ya wanajeshi 180 na 200 katika mahojiano na runinga moja ya Somali Cable TV.
Wapiganaji hao wa al-Shabab wamesema kuwa wanajeshi 100 walifariki.Kenya haijatoa idadi yoyote ya wanajeshi wake waliofariki kufikia sasa.
Rais huyo wa Somalia alikuwa akitetea ziara yake nchini Kenya baada ya hisia kali kutolewa katika mitandao ya kijamii kufuatia shambulio la mgahawa wa Lido Beach katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu mnamo mwezi Januari.
Alisema kuwa ilikuwa muhimu kutoa heshima kwa wanajeshi wa Kenya waliouawa:.
''Wanajeshi wa kigeni hufariki na hatuendi katika mazishi yao.wakati wanajeshi 180 ama 200 wa kenya waliotumwa nchini Somalia na sabab ya kutumwa kwao nchini humo ni kuleta udhabiti kuwaisaidia raia wa Somalia na wanauawa alfajiri moja ,si swala la kawaida kwamba wageni wameuawa.Kile kilichosalia ni kwamba jamaa zao walielezwa kwamba kulikuwa na vita na watu wao wakafariki kutokana na hilo'',alisema Sheikh Hassan Mahmoud.
BBC imewasiliana na maafisa wa jeshi la Kenya ambao bado hawajazungumzia habari hizi.

Jeshi
Mazishi ya wanajeshi waliouawa yamekuwa yakifanyika maeneo mbalimbali Kenya
Baada ya shambulio hilo kutokea tarehe 15 Januari, Rais Kenyatta aliahidi kwamba majeshi ya Kenya yangewaandama waliohusika.

No comments: