Mwanamume aliyetoweka kazini miaka sita Uhispania - LEKULE

Breaking

14 Feb 2016

Mwanamume aliyetoweka kazini miaka sita Uhispania

Garcia
Garcia alikuwa akipokea mshahara kama kawaida
Mtumishi wa umma nchini Uhispania amepigwa faini baada ya kugunduliwa kwamba hakuwa amefika kazini kwa miaka sita.
Amepigwa faini ya €27,000 (£21,000; $30,000).
Joaquin Garcia aligunduliwa baada yake kuanza kutafutwa apewe tuzo ya kutumikia serikali kwa muda mrefu.
Mfanyakazi huyo wa umri wa miaka 69, ambaye kazi yake ilikuwa kusimamia wafanyakazi katika kiwanda cha kushughulikia maji taka mji wa Cadiz, sasa amestaafu.
Amekanusha tuhuma dhidi yake na kusema 'anazingiziwa na kwamba alikuwa anadhalilishwa.
Bw Garcia alilipwa €37,000 kila mwaka kabla ya kutozwa ushuru.
Kampuni hiyo ya maji ilidhani alikuwa akisimamiwa na serikali ya mtaa nayo serikali ya mtaa ilidhani alikuwa akisimamiwa na kampuni hiyo.
Naibu meya aligundua Bw Garcia alikuwa hafiki kazini baada yake kuanza kutafutwa apewe zawadi kwa kutumikia serikali ya mtaa kwa miaka 20.
Faini aliyotozwa inatoshana na mshahara wake wa mwaka mmoja baada ya kutozwa ushuru.
Mahakama imekubali mashtaka dhidi yake na kuagiza alipe faini hiyo.

No comments: