VITAMBUE HAPA VITUO VITAKAVYOZIMA MATANGAZO YAKE USIKU WA SAA SITA JUMAPILI KWA AMRI YA TCRA - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Saturday, 16 January 2016

VITAMBUE HAPA VITUO VITAKAVYOZIMA MATANGAZO YAKE USIKU WA SAA SITA JUMAPILI KWA AMRI YA TCRAMamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo cha Star TVRadio free AfrikaKiss Fm na Uhuru FM kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..

Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.

Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.

Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.==> Vituo vingine vilivyofungiwa ni;
 • Sibuka FM
 • Breez FM
 • Country FM
 • Ebony FM
 • Hot FM
 • Impact FM
 • Iringa Municipal TV
 • Kiss FM
 • Kitulo FM
 • Kifimbo FM
 • Mbeya City Municipal TV
 • Radio 5
 • Radio Free Afrika (RFA)
 • Musa Television Network
 • Pride FM radio
 • Radio Huruma
 • Radio Uhuru
 • Star TV
 • Rock FM Radio
 • Standard FM radio
 • Sumbawanga Municipal TV
 • Tanga City TV
 • Top Radio FM limited
 • Ulanga FM 
Post a Comment