Uthibitisho wa ajali ya msaidizi wa IGP Mangu pamoja na familia yake - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Monday, 4 January 2016

Uthibitisho wa ajali ya msaidizi wa IGP Mangu pamoja na familia yakeHuenda bado haijakufikia taarifa kuhusu ajali ya Askari mmoja ambaye ni msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Ernest Mangu, kilichonifikia ni taarifa kuhusu mazingira ya tukio la ajali hiyo.
Hii ni nukuu ya sentensi ya Kamanda wa Polisi Dodoma >>> ‘Tulimpata mke wa mkaguzi wa Polisi, Gerard Rioba ambaye ni msaidizi wa IGP, baadae tukampata dereva wa gari lao akiwa amefariki… Tumepata miili ya watoto wake wawili, na baadae tukapata mwili wa marehemu msaidizi wa IGP, Marehemu Rioba‘- Kamanda David Misime.
Marehemu alikuwa na mkewe, watoto wake wawili, msichana msaidizi wa ndani, na msaidizi wake… mazingira ya ajali yanaonesha gari ilisombwa na maji katika eneo la Bwawani, Kongwa Dodoma… #RIP.
Post a Comment