Makaburi matano yagunduliwa Bujumbura - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 29 January 2016

Makaburi matano yagunduliwa Bujumbura

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeena picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi.
Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura.
Shirika hilo linaongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku ya tarehe 11,desemba,siku ambayo ilishuhudia machafuko makubwa mjini Bujumbura.
Ripoti hiyo imekuja siku chache kabla ya mkutano wa viongozi wa umoja wa Afrika kukutana kujadili hatima ya mgogoro wa Burundi huko Ethiopia.
Mgogoro wa Burundi ulianza april mwaka uliopita, wakati ambapo raisi Pierre Nkurunzinza alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi kwa awamu ya tatu na kuchaguliwa tena kuwa raisi mwezi july mwaka wa jana.
Post a Comment