Kanisa lenye umbo la kiatu lajengwa Taiwan - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 17 January 2016

Kanisa lenye umbo la kiatu lajengwa Taiwan


Kanisa la kiatu
Kanisa la urefu wa mita 16 lililojengwa kwa kutumia vigae vya glasi linalofanana na viatu vyenye visigino virefu vinavyopendwa sana na wanawake limejengwa huko Taiwan kwa lengo la kuwavutia wanawake zaidi.
Likiwa limejengwa kwa kutumia vigae vya glasi takriban 320,kanisa hilo la rangi ya buluu lina upana wa mita 10 na limegharimu takriban dola 686,000.
Picha iliopigwa juu ya kanisa hilo pia imeonyesha ukubwa wa kanisa hilo pamoja na uzuri wa eneo lililojengwa.
Jumba hilo la kuabudu linatarajiwa kufunguliwa tarehe 8 mwezi Februari tayari kwa mwaka mpya wa Uchina.
kanisa la kiatu Taiwan
Kiatu hicho kimetengezwa na maafisa wa baraza la miji kusini magharibi mwa pwani ,katika eneo moja la kitalii lenya umaarufu mkubwa huko Taiwan.
Lakini Pan Tsuei-ping,msimamizi wa ujenzi huo,ameiambia BBC kwamba kanisa hilo halitatumika kwa huduma za ibada za kila siku bali hafla za harusi.

''Katika mipango yetu,tunataka kulifanya eneo hili kuwa la kuvutia kimapenzi,kila msichana angepanda kutafakari atakapokuwa bibi harusi alisema'', Pan aliiambia BBC.
Post a Comment