Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Tukio
hili limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi
wa Kata hiyo kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mchungaji
Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini
akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya
Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. (P.T)
Diwani wa
Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza James Katoro (CCM)
akihutubia katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa
kumchagua kuwa diwani wao. Aliahidi kushughulikia kero mbalimbali zilizo
katika Kata hiyo ambazo ni pamoja na kero ya maji, ujenzi wa zahanati
na vituo vya afya, miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za msingi na
Sekondari.
Salum
Abdallah Said ambae ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza
katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa
ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba
25,20515.
Kulia ni
Jeremiah Mtoni ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika
mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi
waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Elias
Makaranga (mwenye kinasa sauti) ambae alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani
Katoro katika uchaguzi uliopita akizungumza jambo katika mkutano wa
kuwashukuru wananchi uliofanyika jana.
Wakazi wa
Kata ya Kayenze wakifuatilia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM katika
Kata hiyo wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho katika uchaguzi
uliofanyika Novemba 25, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment