NDEGE ya mafunzo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imepata ajali ikiwa na marubani wawili katika eneo la Silversands, Visiwa vya Bundya, katika Mwambao wa Bahari ya Hindi Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, ilisema marubani hao wanaendelea kutafutwa baada ya kuzama habarini.
Tukio hilo limetokea Oktoba mosi, mwaka huu, saa tatu 3:30 asubuhi ambapo marubani waliopotea ni Luteni Kanali Talkisiyo Ndongoro na Kapteni Gaudence Hamis.
Chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya injini ambapo baada ya marubani kugundua hitilafu hiyo, walifanya juhudi za kujiokoa kwa kutoka katika ndege, kuangukia baharini na kuzama.