Mwana Wa Mfalme Ampinga Platini - LEKULE

Breaking

30 Jul 2015

Mwana Wa Mfalme Ampinga Platini

Aliyekua mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Ali bin Al Hussein amempinga rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini kwa kusema hafai kusimama katika kinyang’anyiro cha kujaza nafasi ya Sepp Blatter kwenye uchaguzi wa mwezi februari mwakani.
Ali bin Al Hussein ambaye ni mtoto wa mfalme wa Jordan, ametoa angalizo hilo baada ya saa 24 kupita, ambazo zilishuhudia Platini akitangaza nia ya kuwania kiti cha uraisi wa FIFA baada ya kupata Baraka kutoka kwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya UEFA mwishoni mwa juma lililopita.
Al Hussein amesema Platini hana sifa zilizo thabit za kuiongoza FIFA ambayo kwa sasa imetapakaa uchafu wa rushwa, hivyo amewataka wadau wa soka duniani kutambua kwamba kuna ulazima kwa baadhi ya viongozi kujipima kabla ya kutangaza nia ya kuwania nafasi kubwa katika taasisi za kidunia.
Hata hivyo Al Hussein hakuweka wazi ni vipi Platini hatoshi katika nafasi hiyo kwa vigezo vya kuzuia rushwa, zaidi ya kusisitiza kuna ulazima kwa baadhi ya watu kujichunguza kwanza kutokana na vitendo vinavyoendelea miongoni mwa watu wanaowazunguuka.

Katika hatua nyingine Al Hussein, bado hajatangaza kama atawania nafasi ya urais kwa mara nyingine tena ama la, hali ambayo inahisiwa huenda ikawa ni hofu kwake baada ya kuona Platini ametangaza nia ya kukitaka kiti cha urais wa FIFA.



No comments: