Rais Magufuli Asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa....Awasili Mjini Dodoma kwa Gari - LEKULE

Breaking

18 Nov 2015

Rais Magufuli Asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa....Awasili Mjini Dodoma kwa Gari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi  majuzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph  Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe.  Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.
====
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
 
Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
 
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma  kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
 
Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU

November 17, 2015

No comments: