11 Nov 2015

CCM yaanza mchakato wa kusaka wenye sifa za kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

CCM
Muonekano wa jengo la Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatangaza Ratiba ya Uchukuaji Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wana-CCM wote wenye sifa husika. 

Ratiba ya mchakato huo ni kama ifuatavyo;-

Wana-CCM wasio Wabunge wanaoomba ridhaa ya CCM kugombea Uspika wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na kuzirejesha Novemba 12, 2015 kabla ya saa Kumi Kamili Jioni.
  1. Kwa wana-CCM ambao ni Wabunge wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoomba kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge hilo, wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na kuzirejesha Novemba 14, 2015 kabla saa Kumi Kamili Jioni.
Fomu hizo zitatolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,  Ndugu Mohamed Seif Khatib.
Imetolewa na:- 
KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA

IDARA YA ITIKADI NA UENEZ

No comments:

Post a Comment