16 Sept 2015

ACT-Wazalendo: Tutamaliza Migogoro ya Ardhi

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, amesema akichaguliwa kuwa rais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, atamaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulimana wafugaji inayoendelea katika mikoa mbalimbali.
 
Mghwira aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika  kwenye Uwanja wa Toboa Tobo, Wilayani Malinyi, mkoani Morogorona kuongeza kuwa, migogoro mingi ya ardhi inayohusisha makundihayo inachangiwa na uongozi mbovu.
 
Alisema uongozi wa CCM umeshindwa kusimamia matumizi bora ya ardhi au kutoa upendeleo kwa kundi moja, hivyo akiwa rais, atahakikisha migogoro hiyo inaisha katika muda mfupi na kuweka viongozi makini ambao hawawezi kupokea rushwa ili kupendelea upande mmoja. 
 
"Baadhi ya wananchi wanashindwa kutumia kilimo ili waondokane na umaskini kutokana na baadhi ya watendaji kutumia migogoro ya ardhikwa lengo la kujinufaisha, hivyo wapigieni kura wagombea wa ACT tuweze kuitatua changamoto hii na kuwaletea maendeleo.
 
"Vipaumbele vyetu viko vinne ambavyo ni elimu, hifadhi ya jamii, afya na uchumi shirikishi ambavyo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania wakiwemo wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, pia tutaanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ili wapate mikopo," alisema.
 
Naye mgombea mwenza, Hamad Musa Yusuph, alisema huu ni mwaka wa mageuzi na ili kuleta maendeleo ya kweli  lazima wakazi wa Malinyi wamchague mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo kwa kuwa CCM  haiwezi kuleta maendeleo kwa miaka mitano ijayo.
 

Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Idaya Usangu, alisema kuna matatizomengi jimboni humo ikiwemo migogoro ya ardhi, ubovu wa barabara unaosababisha wananchi kushindwa kusafiri hasa wakati wa masika kitu ambacho akichaguliwa atakipatia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment