WASIRA AAGIZA WADAU WA SUKARI KUINGIZA SOKONI BIDHAA HIYO BADALA YA KUIFUNGIA GHALANI - LEKULE

Breaking

12 Feb 2015

WASIRA AAGIZA WADAU WA SUKARI KUINGIZA SOKONI BIDHAA HIYO BADALA YA KUIFUNGIA GHALANI

Wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari wakimsikiliza kwa makini maamuzi ya serikali  kuhusu bei ya sukari.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira na Naibu wake (kushoto) Mh.Godfrey Zambi, Bi. Sophia Kaduma Katibu Mkuu (kulia) na Dkt.Yamungu Kayandabila (kushoto) wakifuatilia kwa makini mjadala baina yao na wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Kilimo

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Stephen Wasira  akisisitiza jambo wakati alipokutana na wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari hapa nchini katika ukumbi wa mikutano hapa wizarani.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe Stephen Masatu Wasira amekutana na wadau wa sukari na kutoa tamko la serikali kuhusiana na kupanda kwa ya sukari hapa nchini.
Mhe Wasira amewaagiza wazalishaji na wafanya biashara wa sukari hapa nchini kuingiza sukari sokoni badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu

 Agizo hili la waziri limekuja muda mfupi baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1700/= iliyokuwa ikiuzwa awali hadi shilingi 3000 kwa kilo.

 Aidha hali hiyo ilisababishwa na upungufu ulijiotokeza ghafla baada ya serikali kuthibiti uingizwaji holela wa sukari toka nje ya nchi.

 Upande wa Wadau wameahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha kuwa sukari inapatikana sokoni na kwa bei nafuu.

 Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadu wa sukari itaagiza tani 100000 ili kukabiliana na upungufu unaotokea kila mwaka wakati viwanda vinapofungwa kwa ukarabati.

 “Serikali itatoa kibali cha kuingiza sukari tani 100000 mwezi machi ili kukabiliana na upungufu utakaojitokeza pindi ukarabati” alifahamisha Mhe Wasira.



No comments: