Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesisitiza kuwa mchakato wa Katiba mpya unaendelea vizuri na kwamba muda uliopo unatosha kwa ajili ya zoezi la kampemi pamoja na kupiga kura ya maoni.
Akizungumza katika mahojiano muda mfupi baada ya kukutana na wahariri wa vyombo vya habari, Mwanasheria Mkuu Masaju amewataka wananchi kuondoa hofu juu ya uwezekano wa kufanyika kwa kura ya maoni kwa madai muda uliopo hautoshi kwa ajili ya maamuzi kuhusu Katiba inayopendekezwa kufanyika hapo Aprili 30.
Masaju amesema zoezi la elimu kwa umma, kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kampeni vinaweza kufanyika kwa pamoja ndani ya muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment