Mkazi wa Mwanza Ajishindia Bajaji ya 6 ya Promosheni ya Tutoke na Serengeti - LEKULE

Breaking

12 Feb 2015

Mkazi wa Mwanza Ajishindia Bajaji ya 6 ya Promosheni ya Tutoke na Serengeti



 Bajaji ya sita ya kampeni ya Tutoke na Serengeti, safari hii itaelekea mkoani Mwanza baada ya bwana. Ramadhan Abubakar kutangazwa kuwa mshindi wa Limo Bajaj, kufuatia ushiriki wake yakinifu tangu kuanza kwa kampeni hii.
 
Akiongea kwa njia ya simu, Abubakar  (28) ambaye ni fundi umeme na mkazi wa Nyamagana, Mwanza alielezea furaha yake baada ya kuelezwa na SBL kwamba ameshinda Limo Bajaj mpya katika kampeni ya Tutoke na Serengeti…. “Aisee Mungu ni Mwema,…alitahamaki,… asante sana kwa kunipa habari hii njema sikutarajia kushinda kabisa.”
 
Baada kuulizwa ni kwa namna gani ataitumia bajaji  aliyoshinda katika shughuli zake za kila siku , alisema ataitumia Bajaji hii kwa shughuli za usafirishaji. Mwakazi aliongeza kwamba bajaji hiyo itamsaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato cha familia kwa zaidi ya asilimia  50 huku akiwa na lengo la kujiendeleza kitaaluma kwenye ufundi umeme.
 
Akiongea na vyombo ya habari leo katika makao makuu ya SBL yaliyoko Chang’ombe Dar es salaam, Meneja chapa wa Serengeti Premium Lager Mr. Rugambo Rodney alisema :

"Mshindi wetu wa sita wa  Limo Bajaj nae anatoka nje ya Dar es salaam kuashiria kwamba kampeni hii imepokelewa vizuri mikoani  kinyume na ilivyozoeleka na watu wengi kwamba  kampeni za namna hii ni za wakazi wa Dar tu."
 
Rodney aliongeza kuwa kwa sasa imebaki nafasi moja ambayo ni ya Mtoko wa mbugani huku akiwahimiza wateja kutumia mwezi huu wa wapendanao kuwa “Surprise” na kutoa zawadi ya “Mtoko wa mbugani kwa wenza wao ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. 
 
Kwa upande mwingine ujumbe kutoka BPESA wataalam wa teknolojia ambao katika promosheni hii wanahusika na usambazaji wa fedha kwa washindi kupitia njia ya simu maeneo mbalimbali hapa nchini, imethibitisha kuwalipa fedha taslim washindi wa kila wiki.
 
Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja anatakiwa awe na umri wa miaka 18, anunue Serengeti Premium Lager na aangalie chini ya kizibo ambapo atakutana na namba maalum anazotakiwa kuzituma kwa njia ya sms kwenda  15317. Kadiri unavyoshiriki mara nyingi ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya ushindi.

No comments: