Raia 20 wa kigeni wauawa Bangladesh - LEKULE

Breaking

3 Jul 2016

Raia 20 wa kigeni wauawa Bangladesh


Bangladesh
Watu 20 wote wakiwa raia wa kigeni wameuawa wakati wa shambulio linalodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Islamic State katika mgahawa mmoja nchini Bangladesh,kulingana na maafisa.
Wapiganaji walivamia mgahawa wa Holey Artisan mjini Dhaka jioni siku ya Ijumaa kabla ya vikosi vya usalama kuingia yapata saa 12 baadaye.
Wapganaji sita waliuawa huku mmoja akikamatwa kulingana na msemaji wa serikali.
Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Waathiriwa wengi walidaiwa kutoka Itali na Japan.
Brigedia wa jeshi nchini humo jenerali Asraf Chowdhury alisema kuwa waathiriwa walishambuliwa na silaha kali.BBC

No comments: